MATOKEO YA UTAFITI WA MRADI WA EFLOWS YANASUBIRIWA NA NCHI 10 ZA AFRIKA MICHUZI BLOG at Sunday, March 12, 2023 Na Amina Hezron, Mbeya. Imeelezwa kuwa matokeo ya Utafiti wa Mradi wa Tathimini ya Maji kwa Mazingira (EFLOWS) unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwakushirikiana na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) yanatarajiwa kwenda kutumika kama mfano kwenye nchi kumi za Afrika katikaukanda wa magharibi mwa Bahari ya Hindi ambazo zinakabiliwa na changamotoza uhifadhi kama ilivyo kwenye mto Mbarali. Hayo yameelezwa na kiongozi wa Sekretarieti ya Azimio la Nairobi, Dixon Waruinge wakati alipokuwa akifafanua kuhusu umuhimu wa Mradi wa EFLOWS pamoja na lengo ya ziara yao ya tathimini toka mradi huo kuanza kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Filangali Mwila na maafisa wengine kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira. Amesema kuwa utaalamu wa kuhifadhi maji kwenye mito haupo kwenye nchi nyingi za Afri...