Skip to main content

MATOKEO YA UTAFITI WA MRADI WA EFLOWS YANASUBIRIWA NA NCHI 10 ZA AFRIKA

 

 Na Amina Hezron, Mbeya.

Imeelezwa kuwa matokeo ya Utafiti wa Mradi wa Tathimini ya Maji kwa Mazingira (EFLOWS) unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwakushirikiana na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) yanatarajiwa kwenda kutumika kama mfano kwenye nchi kumi za Afrika katikaukanda wa magharibi mwa Bahari ya Hindi ambazo zinakabiliwa na changamotoza uhifadhi kama ilivyo kwenye mto Mbarali.


Hayo yameelezwa na kiongozi wa Sekretarieti ya Azimio la Nairobi, Dixon Waruinge wakati alipokuwa akifafanua kuhusu umuhimu wa Mradi wa EFLOWS pamoja na lengo ya ziara yao ya tathimini toka mradi huo kuanza kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Filangali Mwila na maafisa wengine kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira.

Amesema kuwa utaalamu wa kuhifadhi maji kwenye mito haupo kwenye nchi nyingi za Afrika ya Mashariki na hivyo ikaonekana uanzishwe mradi huo ambao utasaidia kuongeza elimu na ufahamu juu ya taaluma hiyo.

“kazi kubwa inayofanywa na watafiti hawa hapa Tanzania siyo kazi ya Tanzania peke yake japokuwa inafanyika Tanzania ni kazi ya nchi kumi, elimu bora tutakayoitoa hapa ni lazima tuieneze kwa nchi nyingine ili tukaseme kuwa inawezekana kwasababu watanzania wameweza na wametuonyesha njia na uzuri ni kuwa Prof. Japhet Kashaigili ni mmoja ya wale wanaoeneza elimu hiyo, hivyo tumpe nguvu hapa Tanzania elimu hiyo aipeleke nchi nyingine maana hata sasa anahusika katika kazi kama hiyo huko Madagasca”, alisema Waruinge.

Akieleza sababu za kuchagua mto huo Mtafiti Mkuu wa Mradi EFLOWS kutoka SUA Prof. Japhet Kashaigili amesema kuwa mto Mbarali ni mto ambao awali ulikuwa ukitiririsha maji mwaka mzima lakini miaka ya karibuni mto huo umeanza kukata maji hivyo kuna maswali ya kujiuliza ni nini kinapelekea hali hiyo.

“Hii hali imeleta changamoto ambayo tunajaribu kutafakari kwa sababu tunaiangalia katika upana mkumbwa kwamba serikali ipo katika jitihada kubwa ya uendelezaji wa miradi ya kimkakati kama nchi na moja ni Mradi wa Kufua Umeme wa Mwalimu Nyerere ambapo bila maji mradi huu hauwezi kuwa endelevu na mto Mbarali unachangia maji kwenye bwawa lile lakini sasa mto unakauka hasa eneo la chini”, alieleza Prof. Kashaigili.

Prof. Kashaigili amesema miaka michache iliyopita Mhe. Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan akiwa Makamu wa Rais aliunda kamati ya kitaifa ya kuangalia changamoto hizo na yeye alikuwa ni mmoja wa wataalamu walitoa mapendekezo na maazimio mengi ya mambo ya kufanya na hiki wanachofanya sasa ni sehemu ya kutekeleza mapendekezo yale.

Aidha ameongeza kuwa mradi huo ni wa mfano kwakuwa wana ainisha athari zitokanazo na shughuli za kibinadamu na jinsi ambavyo zinaathiri mtiririko wa maji kwenye mito lakini pia wanaangalia namna ya kupunguza athari hizo kwa kushirikiana na wadau wote walio kwenye maeneo hayo.

Amesema pamoja na utafiti wao, pia wameanzisha vitalu vya miche rafiki wa maji ambapo miche 45,000 imeoteshwa na zoezi la kupanda linaendelea kwenye vyanzo vya maji ambavyo vimeathirika na shughuli za kibinadamu pamoja na kingo za mito ndani ya mita 60 kwenye maeneo mbalimbali ya Wilaya ya Wanging’ombe lakini pia kwenye Wilaya ya Mbarali ili kurudisha uoto wa asili.

Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Filangali Mwila amepongeza kazi hiyo inayofanywa na watafiti hao kwa kushirikiana na Serikali katika kusaidia kupatikana kwa ushahidi wa kisayansi unatokana na tafiti ili kuweza kuyapa nguvu maamuzi yoyote yanayofanywa na Serikali katika bonde hilo muhimu linalotegemewa na miradi ya kimkakati.

Aidha mkuu huyo wa Wilaya ya Mbarali amesema wao kama viongozi na Serikali wanatambua umuhimu wa Bonde hilo kama chanzo kikubwa cha maji kuelekea kwenye miradi mikubwa ya kufua umeme lakini pia wanatambua uhitaji wa maji kwa wananchi katika kufanya shughuli za kilimo lakini maamuzi yoyote yanayofanywa yazingatie maslahi mapana ya Taifa kiuchumi na sio watu wachache ambao wanaweza patiwa maeneo mengine ya kufanya kilimo na wakaendelea kuishi na kustawi.

“ Sisi kama Serikali ya wilaya tupo tayari kutoa ushirikiano wa hali na mali katika kuhakikisha matokeo ya utafiti huu yanapatikana na utaalamu wake unatumika katika kufanya maamuzi sahihi kuhusu bonde hili na mito yake na hapa ningependa kuomba wataalamu wetu mtoe ushauri vyema, mfano swala la watu kuondoka kwenye bonde lilikuwa wazi lakini baadae likatolewa tamko la kuwacha walime kwa mwaka mmoja ndio waondoke lakini mimi natamani tunapoamua kufanya maamuzi magumu tufanye maamuzi magumu kwa faida na maslahi mapana ya taifa letu”, alifafanua Mhe. Kanali Mwila.

Aidha amesema kauli hiyo inaweza kuleta athati kubwa zaidi kwenye eneo hilo kwani kwa kuwa wanajua wameambiwa walime msimu mmoja ndio waondoke wanaweza kuongeza maeneo ya kilimo ili wavune zaidi kupata faida kubwa lakini matokeo yake uharibifu ukawa mkubwa kwakuwa wanajua wanaondoka.

Mradi huu wa Utafiti unatekelewa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kushirikiana na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na kutekelezwa katika bonde la mto Rufiji ndani ya dakio la mto Mbarali kwa ushirikiano na Bodi ya Maji ya mto Rufiji, jumuiya za watumia maji, Wakala wa Huduma za Misitu (TFS), Wilaya ya Mbarali na Wanging`ombe na jamii, kwa ufadhili wa program ya Mazingira ya Umoja wa Mataifa, UNEP na kutekelezwa kupitia Sekretarieti ya Azimio la Nairobi.
 
Kiongozi wa Sekretarieti ya Azimio la Nairobi, Dixon Waruinge akisisitiza jambo wakati wa ziara yake kutembelea maeneo ambayo yanatekeleza kazi mbalimbali za utafiti wa mradi wa EFLOWS.
 
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Filangali Mwila akisisitiza jambo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi wa EFLOWS katika Wilaya yake.
Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Filangali Mwila akisisitiza jambo mara baada ya kupokea taarifa ya utekelezaji wa mradi wa EFLOWS katika Wilaya yake.
 
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Mbarali Mwl. Missana Kwangura akieleza mikakati ya Halmashauri yake katika kuunga Mkono juhudi za Mradi huo katika uhifadhi wa vyanzo vya maji na mito.
Mkurugenzi Msaidizi wa Ofisi ya Makamu wa Raisi Mazingira Bw. Thomas Bwana kitoa salamu za Mkurugenzi ofisi ya makamu wa Raisi Mazingira wakati wa kikao cha pamoja na Jumuiya ya MBUMTILU.
 
Watafiti wa mradi wa EFLOWS, Maafisa kutoka Ofisi ya Makamu wa Riasi Mazingira, Maafisa kutoka Sekretarieti ya Azimio la Nairobi, na Jumuiya ya watumia maji ya MBUMTILU wakijadiliana jambo wakati wakiangalia moja ya chanzo cha maji kilichoharibiwa na shughuli za binadamu na sasa kimepandwa miti rafiki wa maji kurudisha uoto wake wa asili.

Comments

Popular posts from this blog

EFLOWS Project Research Results Workshop held in Mbarali district September 07, 2023 at Jumbo Hotel - Rujewa

  Calvin Gwabara and Amina Hezron The Government has commended the Sokoine University of Agriculture (SUA) and the National Environment Management Council (NEMC) for their efforts to help restore natural vegetation to water sources as well as conducting research and providing results that will help the Government make the right decisions. Mbarali District Commissioner, Hon. Col. Denis Mwila speaking during the opening of the Workshop This has been explicated by the Mbarali District Commissioner, Hon. Col. Denis Mwila during the opening a workshop to present the results of the project's research on the Sustainable Catchment Management through Enhanced Environmental Flows Assessment and Implementation for the protection of the Western Indian Ocean from land-based sources and activities in Tanzania (EFLOWS) held in Rujewa, Mbeya Region. "There is a big security impact that seems to be coming to the fore now due to the destruction of the environment but if you look carefully a...

Capacity Building on Environmental Flows Assessment in WIO Countries

Capacity Building on Environmental Flows Assessment in WIO Countries District Commissioner for Mbarali (center seated) poses with Participants for group photo Training on Environmental Flows Assessment in WIO Countries physically was held on 19 th to 24 th September, 2022 at Rufiji Basin Water Board Office in Mbarali, Tanzania. Virtually participants from South Africa, Mozambique, Seychelles, Comoros Islands, Mauritius, Madagascar, Kenya and Somalia countries participated in the sessions. Various topics were presented in the training sessions such as: ·          Environmental Flows and its Importance, ·          Situation analysis, ·          Science of Environmental Flows, ·          E-flows Assessment Methodologies, ·          Environmental Flow Frameworks, ·  ...