Skip to main content

EFLOWS Inception Workshop Held on 29th July 2021 in Mbarali District, Mbeya

 

NEMC Washirikiana Na SUA Kuzindua Mradi wa Utafiti Wilayani Mbarali Mkoani Mbeya

 

Na

Calvin Gwabara - SUA

 

Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune ambaye ni Mgeni Rasmi, akiongea wakati wa uzinduzi wa  Mradi  unaoratibiwa na NEMC na SUA, wa utafiti wa usimamizi endelevu wa madakio ya maji kupitia tathimini ya kuimarisha mtiririko wa maji kwa mazingira na utekelezaji wake katika kulinda Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi kutokana na athari za shughuli za kibinadamu, Tanzania (EFLOWS). Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Maji Bonde la Rufiji Wilayani Mbarali.

 

Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Taifa la Usimamizi na Uhifadhi wa Mazingira (NEMC) ambaye ni Meneja wa Utafiti kutoka NEMC  Bi. Rose Salema Mtui akisoma hotuba ya ukaribisho katika uzinduzi  wa mradi huo kwa niaba ya Mkurugenzi Mkuu wa NEMC Dkt. Samwel Gwamaka.

Sehemu ya Wajumbe waliohudhuria katika uzinduzi wa Warsha ya uzinduzi wa Mradi unaoratibiwa na NEMC na SUA wa utafiti wa usimamizi endelevu wa madakio ya maji kupitia tathimini ya kuimarisha mtiririko wa maji kwa mazingira na utekelezaji wake katika kulinda Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi kutokana na athari za shughuli za kibinadamu, Tanzania (EFLOWS). Uzinduzi huo umefanyika Wilayani Mbarali.


Mgeni Rasmi katika uzinduzi huo ambaye ni Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mhe. Reuben Mfune akiwa katika picha ya pamoja na Wajumbe waliohudhuria warsha ya uzinduzi ya mradi wa utafiti wa usimamizi endelevu wa madakio ya maji kupitia tathimini ya kuimarisha mtiririko wa maji kwa mazingira na utekelezaji wake katika kulinda Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi kutokana na athari za shughuli za kibinadamu, Tanzania (EFLOWS).

…………………………………………………..

Ni jukumu la kila mdau kama vile serikali za Mitaa, wakulima, wafugaji, jumuia za watumiaji maji, watunzaji wa mazingira na taasisi binafsi kuhakikisha kwamba rasilimali maji zote zinalindwa kikamilifu kwa ajili ya uendelevu wa madakio ya maji na maisha kwa ujumla.   

Hayo  yamesemwa  na Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Mh. Reuben Mfune ambaye alikuwa Mgeni Rasmi wakati wa warsha ya  uzinduzi wa Mradi wa utafiti wa usimamizi endelevu wa madakio ya maji kupitia tathimini ya kuimarisha mtiririko wa maji kwa mazingira na utekelezaji wake katika kulinda Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi kutokana na athari za shughuli za kibinadamu, Tanzania (EFLOWS). Uzinduzi huo umefanyika katika ukumbi wa Ofisi ya Maji Bonde la Rufiji, Wilayani Mbarali katika Mkoa wa Mbeya.

Vilevile Mheshimiwa Mfune,  ametoa  shukrani kwa Shirika la Umoja wa Mataifa la Uhifadhi wa Mazingira (UNEP) kwa ufadhili wa kifedha katika mradi huo, pia Sekretarieti ya Azimio la Nairobi (Nairobi Convection Secretariat) ambayo ni msimamizi wa utekelezaji. Pamoja na Waratibu wa mradi huo kutoka Baraza la Taifa la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwa kujitoa kwao kutekeleza mradi huu ambao ni mojawapo ya miradi iliyopo katika nchi zilizo kwenye Mpango Mkakati wa nchi za Magharibi mwa Ukanda wa Bahari ya Hindi 

Aidha, amesema kuwa, anafurahi  kuona kwamba masuala ya mazingira kama vile umwagiliaji, kilimo kandokando ya kingo za mito, ufugaji wa mifugo ndani ya kidakio cha mto Mbarali na Bonde la Rufiji pamoja na ongezeko la watu, vinasimamiwa kwa uhifadhi kamilifu wa eneo la Magharibi mwa Ukanda wa Bahari ya Hindi. Na muhimu zaidi kwa ajili ya mtiririko endelevu wa maji kuelekea Mradi wa kufua umeme wa Mwalimu Nyerere (Julius Nyerere Hydro Power Project  – JNHPP).

Naye Mkurugenzi Mkuu wa NEMC katika hotuba yake  ya ukaribisho kwa mgeni Rasmi iliyosomwa kwa niaba yake na Meneja wa Utafiti-NEMC Bi. Rose Salema Mtui amesema kuwa,  NEMC kwa kushirikiana na taasisi za kitaaluma/utafiti zimekuwa zikitengeneza miradi/programu  na kufanya tafiti na mojawapo ni kama mradi huo uliozinduliwa kwa lengo la kutatua matatizo mbalimbali ya kimazingira. 

“Kupitia mradi huu, utekelezaji wa mtiririko wa maji kwa mazingira (env. flow) ni muhimu sana kwa uendelevu wa ikolojia ya mto; na natumaini wadau wote na Serikali kwa ujumla watakuwa tayari kutoa ushirikiano mkubwa kuhakikisha malengo ya mradi huu yametimia” alisema.

Akiongea katika warsha hiyo ya Uzinduzi Mkurugenzi wa Shahada za Juu Uhawilishwaji wa Teknolojia za Kitafiti kutoka Chuo cha Sokoine cha Kilimo – SUA, Profesa Esron Karimuribo  amesema kuwa kuna uharibifu mkubwa wa vyanzo vya maji nchini na umetokana na shughuli mbalimbali za kibinadamu, kama vile ukataji miti, uchomaji misitu, kilimo pembezoni mwa vyanzo vya maji, uchimbaji madini, ufugaji na uchepushaji wa maji. Hivyo basi katika mradi huo ambao utafanyika katika wilaya ya Mbarali  na wilaya hiyo imechukuliwa kama kianzio tu.

Mradi huo wa utafiti wa usimamizi endelevu wa madakio ya maji kupitia tathimini ya kuimarisha mtiririko wa maji kwa mazingira na utekelezaji wake katika kulinda Ukanda wa Magharibi mwa Bahari ya Hindi kutokana na athari za shughuli za kibinadamu, Tanzania (EFLOWS) unaratibiwa na Baraza la Taifa la Hifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) na Chuo cha Kilimo cha Sokoine (SUA).




Comments

Popular posts from this blog

Mapping Water Sources in the Upper Mbarali River Sub-Catchment

  FIELD REPORT NOVEMBER 2021 Mapping Water Sources in the Upper Mbarali River Sub-Catchment One of the Mbarali River source of water in Waging'ombe district Njombe Region   Introduction Mbarali river is one of sub-catchment within Rufiji River Basin in the Southern Highland of Tanzania facing ongoing degradation due to land use change, poor institutional management and climate change. Degradation and poor management of water sources have affected river flows in both quantity and quality with devastating impacts on the downstream including the coastal and marine ecosystems through increased inflow of nutrients, sediment deposits, and variation of flow regimes. The exponential growth of water demand catalyzed by the increase of anthropogenic activities and population growth increase the pace of environmental degradation within the sources and along the entire river to the downstream. There are initiatives which have been taken for water sources management such as establishment ...

MATOKEO YA UTAFITI WA MRADI WA EFLOWS YANASUBIRIWA NA NCHI 10 ZA AFRIKA

  MATOKEO YA UTAFITI WA MRADI WA EFLOWS YANASUBIRIWA NA NCHI 10 ZA AFRIKA MICHUZI BLOG at Sunday, March 12, 2023    Na Amina Hezron, Mbeya. Imeelezwa kuwa matokeo ya Utafiti wa Mradi wa Tathimini ya Maji kwa Mazingira (EFLOWS) unaotekelezwa na Chuo Kikuu cha Sokoine cha Kilimo (SUA) kwakushirikiana na Baraza la Taifa la Uhifadhi na Usimamizi wa Mazingira (NEMC) yanatarajiwa kwenda kutumika kama mfano kwenye nchi kumi za Afrika katikaukanda wa magharibi mwa Bahari ya Hindi ambazo zinakabiliwa na changamotoza uhifadhi kama ilivyo kwenye mto Mbarali. Hayo yameelezwa na kiongozi wa Sekretarieti ya Azimio la Nairobi, Dixon Waruinge wakati alipokuwa akifafanua kuhusu umuhimu wa Mradi wa EFLOWS pamoja na lengo ya ziara yao ya tathimini toka mradi huo kuanza kwa Mkuu wa Wilaya ya Mbarali Kanali Denis Filangali Mwila na maafisa wengine kutoka Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira. Amesema kuwa utaalamu wa kuhifadhi maji kwenye mito haupo kwenye nchi nyingi za Afri...

EFLOWS Project Researchers continue with the Wet season Data collection in the Mbarali River

  By Placid Kabalo Researchers from Sokoine University of Agriculture (SUA) in collaboration with Researchers from the National Environmental Management Council (NEMC) and Researchers from the Rufiji River Basin (RBWB), have met for four days in Rujewa town in Mbarali District in Mbeya Region to collect various Research Data in looking at the ecosystem of the Mbarali River. The Mbarali River is one of the rivers that flows into the Great Ruaha River whose waters flow into the Rufiji River and into the Indian Ocean. Botany researchers collecting data Researcher collecting samples of insects in the Mbarali River Hydrologists collecting various data within the Mbarali river Various species of fish were caught from the Mbarali River for research